Baada ya kuacha kazi BBC, Salim Kikeke afunguka atakachokuja kufanya Tanzania

 

Baada ya kuacha kazi BBC, Salim Kikeke afunguka atakachokuja kufanya Tanzania

Mwandishi nguli wa habari nchini, Salim Kikeke amesema kwamba anao mpango wa kurejea nyumbani nchini Tanzania huku akiwa na nia ya kuendelea na shughuli za uandishi wa habari akisema kwamba ni fani ambayo inaishi ndani ya damu yake.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei 3, 2023, wakati akizungumza kwa njia ya mtandao kupitia taarifa ya habari ya EATV Saa 1 ya East Africa TV 


"Mimi nina hamu kubwa sana ya kurejea nyumbani Tanzania na kuja kusaidia taifa langu na sekta nzima ya uandishi wa habari, uzoefu nilioupata natamani sana kuja kufanya kazi na wanahabari wachanga na waliopo kazini sasa hivi na tukabadilishana mawazo na kuelekezana," amesema Salim Kikeke


Aidha Kikeke ameongeza kuwa, "Mimi narudi nyumbani kama mwandishi wa habari na nitakuwa nafanya shughuli hizo, lakini kwa sasa nataka nichukue mapumziko mafupi, nitakapotoka kwenye mapumziko nitaamua hasa nafanya nini lakini uandishi wa habari hautanitoka kamwe kwenye damu yangu,".


Salim Kikeke ambaye alikuwa akitangaza Dira ya Dunia ya BBC Swahili, alitangaza kuondoka BBC kwa ridhaa yake mwenyewe mnamo Aprili 28, 2023.


Comments:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad