Bakhresa 'Azam TV ilianza Kama Mzaha Mzaha Hivi'


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Azam Media LTD Abubakar Bakhresa katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo ameelezea chimbuko la kuzaliwa kwa kituo cha televisheni cha #AzamTV akidai Azam TV ilianza kimzaha tu.

“Tulianza kimzaha mzaha hivi, tuliona tunapata tabu kutazama mechi za timu yetu ya mpira wa miguu ya Azam ikicheza live. Tukajaribu kutafuta njia ya kutazama mechi zetu live maana tulihisi kuwa tumezidiwa na wenzetu.” amesema Bakhresa

“Mechi zilizokuwa zinarushwa zilikuwa mbili tu za Simba na Yanga na tuliona mpira wa Tanzania unaweza kuwa biashara tukaona ipo haja ya kuwekeza kwenye hii biashara ukizingatia Mpira kwetu Tanzania imemuwa sehemu ya utamaduni wetu.”

Adha Bakhresa ameeleza sababu za kwa nini kampuni hiyo iliamua kuwekeza katika mradi wa minara ya ardhini inayorusha matangazo ya televisheni kwa njia ya antena (DTT) na kubainisha kuwa iliwalazimu kuwa leseni ya DTT ili kuonesha local Channels kwa kipindi hicho sheria za Nchi zilitaka lazima uwe na leseni hiyo ili kuonesha channel za ndani (local channels).


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad