BAWACHA waandamana, polisi wawapa ulinzi mzito



HATIMAYE Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) leo Alhamisi wamekusanyika kwenye viwanja vya posta ya zamani jijini Dar es salaam na kuandamana kushinikiza Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kuwaondoa wabunge 19 ambao walifukuzwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Maandamano hayo ya wanawake wa Chadema yamejiri huku Jeshi la Polisi likiimarisha ulinzi kuzunguka viwanja hivyo ikiwa ni wiki tatu zimepita tangu jeshi hilo lilipozuia maandamano ya Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo waliotaka kuandamana kushinikiza hatua zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa wa ubadhirifu waliotajwa kwenye ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).

Maandamano hayo ya amani yalipangwa kuanzia Manzese hadi Ikulu kuonana na Rais Samia Suluhu Hassan na kumfikishia ujumbe wa kutokukubaliana na ubadhirifu wa fedha za umma uliofanywa, kwa mujibu wa ripoti ya (CAG) ya kila mwaka.

Taarifa iliyotolewa jana Jumatano na Katibu Mkuu wa Bawacha Catherine Ruge ilieleza kuwa Jeshi la Polisi limewaruhusu kwa kuwa maandamano hayo ni ya amani, hivyo watakuwepo kuhakikisha kuna amani, utulivu na usalama.

Maandamano hayo yameanzia Posta ya zamani na kuhitimishwa katika ofisi ndogo za Bunge zilizopo mtaa wa Shaban Robert jijini Dar es Salaam.

Tarehe 7 Mei 2023 mwaka huu Baraza hilo lilitangaza kufanya maandamano hayo lakini siku mbili baadae walitangaza kusogeza mbele maandamano hayo hadi tarehe 11 Mei 2023, kutokana na barua waliyoipeleka polisi kuomba ulinzi, kukosewa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad