Breaking: Kiwanda Cha Jambo Plastic Kinawaka Moto Vingunguti


Moto mkubwa umezuka mchana huu katika Kiwanda cha kuzalisha plastiki kiitwacho Jambo 11 kilichopo eneo la Vingunguti Jijini Dar es salam na hadi sasa unaendelea kuwaka kiwandani hapo.

Juhudi za kuuzima moto huo ambao bado chanzo chake hakijajulikana zinaendelea

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema hakuna madhara kwa Binadamu yaliyotokea kutokana na moto uliozuka Kiwanda cha kuzalisha plastiki cha Jambo 11 kilichopo Vingunguti Jijini Dar es salam lakini mashine na malighafi zimeungua na hadi sasa magari ya Zimamoto tisa yapo eneo la tukio kuendeleza mapambano ya kuuzima moto huo.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ilala, Elisha Mugisha amenukuliwa akisema “Malighafi inayotumika kutengeneza plastiki na mashine zinazozalisha ndizo zinazoungua, tulichofanya ni kuzuia mashine ambazo hazijaathirika zisiungue na tumedhibiti moto usiende ghala jingine"

"Hapa tuna magari ya kuzimia moto tisa tunapokezana maji yakiisha wengine wanafuata Airport, tunapambana na kuzima moto kwanza, tukimaliza tutaanza uchunguzi kujua chanzo cha moto huu ni nini, kuna mashine kama saba zimeungua, hakuna Mtu aliyeumia au kupoteza maisha"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad