Chalamila Aanza Kazi na Moto Dar, Aingia Mtaani Kutathmini


Chalamila
Chalamila

Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameanza kazi rasmi kwa kupita kwenye maduka mbalimbali jijini hapa, ili kuangalia athari iliyosababishwa na mgomo wa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo.

Chalamila amefanya ziara hiyo leo Mei 16, 2023 ikiwa ni siku moja tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa, na hivyo kumuamisha kutoka Kagera ambako amehudumu kwa miezi nane.

Katika ziara hiyo amesema, ingawa hajaingia ofisini ametamani kujua mtaani watu wanasema nini, maeneo mengi aliyopita kinacholalamikiwa hasa ni kero zihusuzo kodi na utoaji wa risiti za kielektroniki.

Amesema eneo lingine ni idara ya forodha imeweka viwango vikubwa vya kodi hasa kwa vitenge pamoja na ufuatiliaji kuwa mkubwa jambo linalokwamisha biashara zao.


“Hii inamaana ya ufuatiliaji wa wateja wote waliolipa kodi bandarini, lakini jambo lingine ni kuwepo kwa kamata kamata kwa wafanyabiashara Kariakoo na kuwakosesha uhuru na kuwasumbua wateja hasa wanaotoka nchi za Congo, Zambia na nyinginezo,”


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akipanda usafiri wa Bajaj leo Jumanne Mei 16, 2023 jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja baada ya kuhamishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutoka Kagera.
“Pia utumiaji wa wafanyakazi wanafunzi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambao inasemekana wana uwezo mdogo wa kuweza kukabili ili huduma kwa wateja kati ya mteja na mtu wa TRA,” alisema Chalamila.

Chalamila ambaye ameonekana kwenye picha kadhaa akiwa kwenye bajaji usiku amesema, kama mtanzania amepita na kujionea kile kinachoendelea ili wakati wa kikao cha Waziri Mkuu na wafanyabiashara, kujua tatizo ni nini.


Mei 16, 2023 Rais Samia aliwabadilisha vituo vya kazi wakuu wa mikoa wanne ambapo Chalamila amepokea kijiti hicho kutoka kwa Amos Makalla ambaye amehamishiwa mkoa wa Mwanza, katika kipindi ambacho mgomo wa wafanyabiashara wa Kariakoo ukiendelea wakilalamikia kodi mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad