Dida Shaibu Ashindwa Kuvumilia 'Kajala unamharibu mwenyewe mtoto wake Paula'

 

Dida Shaibu Ashindwa Kuvumilia 'Kajala unamharibu mwenyewe mtoto wake Paula'

Mtangazaji Staa wa Wasafi FM, Dida Shaibu ameamua kufunguka na kumtema nyongo Mwigizaji Staa wa Bongomovie Kajala Masanja kufuatia mwenendo wa malezi mabovu na kumhamasisha mwanae atoke na wanaume wawili kwa mpigo ili waweze kujipatia pesa.


Hii imekuja baada ya kusemeka kwamba licha ya Paula kuwa na Marioo kajala alimuita Rayvanny Bagamoyo ili akakutane na Paula wakati huohuo akijua kabisa Paula na Rayvanny walishatengana na Paula yupo kwenye mahusiano na mwanaume mwingine ambaye ni Marioo.


Kwa uchungu Dida amesema, kinachofanywa na Kajala siyo sahihi na ikiwa anafanya hivyo kujitafutia pesa basi kuna njia nyingine nyingi nzuri za kupata pesa ya halali kuliko hiyo anayoitumia, amesema mwenye shida siyo Paula bali ni mama yake ambaye anashindwa kumpa mtoto malezi bora na ya hekima badala yake amekuwa mstari wa mbele kumhusisha na mambo maovu.


"Kajala ndugu yangu kama unanisikia ngoja nikwambie, ukilipoea kwa uzuri ni wewe na ukilipokea kwa shali pia familillah, Kajala mtoto unamharibu mwenyewe, wewe ndiye unafanya mtoto aonekane haeleweki, unajua kabisa mwanao na Rayvanny hawako pamoja na mwanao yuko na Marioo kwasasa ambapo hata wewe unashinda kwa Marioo na unacheza nyimbo zake kila siku"


"Inakuwaje unampigia simu Rayvanny usiku wa manane aje bagamoyo mnakoshuti eti aje amliwaze binti yako, inaingia akilini kweli? kulikuwa na ulazima gani wa kumtumia Rayvanny kwenye hicho kipindi chenu wakati unajua kabisa kwa kufanya hivyo unamuumiza Fahyma na mwanae.


"Kwa nini usingemtumia Marioo ambaye ndie mkwe wako kwa sasa, wewe ndie ulitakiwa kuwa mstari wa mbele kumkanya binti yako aache ukaribu na Rayvanny kwani huoni mnavyotukanwa huko mitandaoni??, badala yake mmeenda kuwatafutia na tenti kabisa walale usiku, badilika," amesema Dida Shaibu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad