Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amekutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono na kumchafua mwandishi E. Jean Carroll katika duka Kuu la Manhattan katika miaka ya 1990 na ametakiwa kumlipa fidia ya dola milioni 5.
Carroll alimshtaki Trump akimshutumu kwa madai ya ubakaji katika miaka ya 1990 na kumchafua mwandishi huyo kwa kuita akaunti yake "uzushi."
Trump ambaye ni mgombea Urais wa 2024, amekuwa akipinga madai ya Carroll mara kadhaa huku akikashifu hukumu hiyo kwenye tovuti yake ya mtandao wa kijamii muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutolewa.
“SINA WAZO KABISA HUYU MWANAMKE NI NANI. HUKUMU HII NI AIBU - MUENDELEZO WA UWINDAJI MKUBWA WA MCHAWI WA WAKATI WOTE!” aliandika kwenye Truth Social Bw.Trump.
Kufuatia hukumu hiyo, Trump anakuwa Rais wa kwanza wa zamani kupatikana na hatia ya kiraia kwa makosa ya ngono.
Msemaji wa kampeni ya Trump alisema katika taarifa yake, "Usifanye makosa, kesi hii yote ya uwongo ni jitihada za kisiasa zinazomlenga Rais Trump kwa sababu sasa yupo mstari wa mbele kwenye mbio za kuwa Rais wa Marekani.”
#KitengeUpdates