Eng. Hersi aapa kumshusha Yanga straika kinara wa Afrika Kusini

Eng. Hersi aapa kumshusha Yanga straika kinara wa Afrika Kusini


Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. hersi Said amesema kuwa msimu ujao watamsajili mshambuliaji kinara wa Ligi ya Afrika Kusini (PSL) ili kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya michuano ya ya ndani na Kimataifa.


Hersi amesema hayo wakati akihojiwa na mwandishi nguli wa habari nchini Afrika Kusini jana.


"Nitahakikisha ninampata mchezaji mmoja wa Afrika Kusini, hii sio kwa sababu ya mashabiki bali ni kwa sababu za kiufundi. Atakuwa ni mshambuliaji kinara wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini.


"Siwezi kumtaja jina wala klabu kwa sababu ninaheshimu mikataba ya wachezaji na timu zao. Tunaona tunaopkwenda Congo ama nchi nyingine ambazo wachezaji wetu wanatoka tunapata sapoti kubwa, kwa hiyo hata hapa Afrika Kusini tutafanya hivyo," alisema Hersi.


Kwa upande wake, Msemaji wa Klabu ya Yanga, Ally Shaban Kamwe wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari hapa nchini amesema.


“Rais wa yanga, Eng. Hersi wakati akizungumza jana na mmoja wa waandishi nguli hapa Afrika Kusini, Robert Marawa alisema kuwa yanga itasajili mshambuliaji kinara (top striker) wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu huu, amesisitiza top striker wa PSL anayefanya vizuri sasa hivi, tunawaachia wachambuzi wachambue.


“Nendeni Google, lakini mjue mshambuliaji kinara wa Sauzi kwa sasa, mashine ya mabao itatua Tanzania msimu ujao kukiwasha na Wananchi. Ukichukua furaha tuliyo nayo, ukajumlisha na mabao ya top straiker wa Sauzi anayekuja Yanga msimu ujao, tutakuja kupata magonjwa kama hatutafanya mazoezi.


“Tukifunga tutakuwa tunacheza Amapiano tu kwenda mbele, nasemaje… goli la kwanza tunatetema, goli la pili tunacheza Amapiano tu,” amesema Ally Kamwe.


Kwa Ligi ya Afrika Kusini (PSL), Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns na Khanyisa Mayo wa Cape Town City FC ndiyo anaongoza kwa mabao wakiwa na magoli 12 akifuatiwa na Ranga Chivaviro wa Marumo Gallants mwenye mabao 10.


Bradley Grobler wa SuperSport United SuperSport United, Etiosa Ighodaro wa Chippa United Chippa United, Monnapule Saleng wa Orlando Pirates wote wana mabao 10 kila mmoja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad