Kuanzia msimu huu wa mashindano ya CAF, mechi za fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho barani Afrika zimerejeshwa katika mtindo wa nyumbani na ugenini
Kwa misimu kadhaa iliyopita, mechi za fainali zilipigwa katika uwanja huru unaopendekezwa kufuata vigezo walivyojiwekea CAF
Hata hivyo baada ya fainali kati ya Al Ahly dhidi ya Wydad iliyopigwa Morocco na Al Ahly kuwasilisha malalamiko yao CAF kupinga mechi ya fainali kupigwa katika moja ya klabu iliyotinga fainali, utaratibu umebadilishwa tena na kurejeshwa kama zamani
Kama Yanga itatinga fainali, itakuwa na mechi mbili za kusaka ubingwa wa Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas au USM Alger