Familia ya Lemutuz Yafuguka 'Ameacha Mke na Watoto Wawili'

 

Familia ya Lemutuz Yafuguka 'Ameacha Mke na Watoto Wawili'


Familia ya Lemutuz Yafuguka 'Ameacha Mke na Watoto Wawili'

Dar es Salaam. Familia ya William Malecela (Le Mutuz) imesema mpendwa wao ameacha mke na watoto wawili lakini hawajafanikiwa kuwepo kwenye mazishi yake.

 Le Mutuz alifariki jana na leo Jumatatu anaagwa kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam kisha mwili wake utasafirishwa kwenda Dodoma kwa maziko yatakayofanyika Jumatano.

Akisoma wasifu wa marehemu, mdogo wake Samwel John Malecela alisema kaka yao alizaliwa Machi 25, 1961 mkoani Dodoma akiwa ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya John Malecela.

"Alisoma shule ya msingi kabla ya kuhamia mjini Dodoma na kujiunga na Sekondari ya Majengo.

"Hata hivyo kwa asilimia kubwa alikuwa mwanamitandao hivyo wengi mnamfahamu, kama familia tutasoma wasifu wake kwa ufupi," amesema Samwel.

Amesema baada ya kuhitimu sekondari alikwenda Marekani ambako aliendelea na elimu na kupata shahada.

"Alirudi Tanzania mwanzoni mwa mwaka 2000 na kuendelea na kazi binafsi ikiwamo za online.

"Alioa mke na ana watoto wawili, Agapeo na Noela ambao wanaishi Marekani, leo hawapo hapa lakini kwa baadaye tunategemea kuwa nao," amesema.

Amesema kaka yao tangu 2015  alikuwa akisumbuliwa na moyo na alipata matibabu India na kisha kuendelea na kutibiwa JKCI aliporejea nchini.


"Mei 14 alipata shida na kupelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja, wakati akipatiwa matibabu iligundulika tayari alikuwa amefariki," amesema mdogo huyo wa marehemu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad