Haji Manara Awashukia Wachambuzi Uchwara na Wanaopiga Simu Kutaka Kuleta Waganga wa Kienyeji Kambini Yanga

 

Haji Manara Awashukia Wachambuzi Uchwara na Wanaopiga Simu Kutaka Kuleta Waganga wa Kienyeji Kambini Yanga
Haji Manara

Ameandika Haji Manara: 

Sehemu ya Pili ya Mawazo yangu kuelekea mechi ya fainali ya YANGA vs USM ALGIERS

Tunajua fika Mafanikio ya @yangasc ni Mafanikio ya Nchi na heshma kwetu Watanzania, lakini bado haitupi fursa ya kujiweka kwenye presha ya aina yoyote, tuwaone Wachezaji tayari ni mashujaa na mzigo mzito washahangaika nao, Kiuhalisia Kushinda kikombe hiki ni zaidi ya Bonus.


Labda ningetamani Mh. Rais wetu Mama @samia_suluhu_hassan siku chache kabla ya mechi aongee na Wachezaji wetu hata Kwa njia ya Simu iwapo kama itampendeza, hiyo itakuwa ni zaidi ya hamasa na sio Presha.


Kwanza Mama yetu keshaonyesha kuunga mkono kwa kila hali ili kuziwezesha Team zetu zifanye vzuri kimataifa, ikitokea akafanya hivyo itakuwa ni kitu chenye chachu kubwa kabla ya fainali hiyo kubwa zaidi kuwahi kufanyika Benjamin Mkapa Stadium.


Lakini ukiachana na Presha hizo zipo Presha toka kwetu wenyewe Wanachama, ikiwa kila Mwanachama au Mshabiki atakuwa anataka mawazo yake ndio yafanyiwe kazi na Uongozi tutaharibu, tuwaache Viongozi na Mipango yao, kuelekea hii mechi tubaki njia kuu ya kwenda uwanjani kushangilia tu, kupiga piga Simu na kutuma msg za eti kuna Mganga mpya toka Nyantuzi au Ufilipino, ni kuwapa Presha Viongozi, kama una mganga mahiri wa kutusaidia Ruksa kwa imani yako, lakini kuwapa Presha Hersi @caamil_88 na @arafat__ah ya lazma mganga wako atumike sio sawa.


Mwisho


hatutarajii kuona Wachambuzi wanatuharibia mood ya mechi kwa predictions zao za kuwavunja moyo Wachezaji wetu, wasijitie Uungu Mtu, Wachezaji wanasoma mitandao, muwaache walau tumalize hii game , Tukishinda hiki kikombe hata nyinyi sokoni mtasikika, Hii ni fahari ya kila mmoja wetu nchini.


Acheni kiki japo kwa siku chache, leteni mawazo positive kwa interest ya nchi, kosoeni ikibidi Kwa heshma, mna nafasi yenu pia lakini mnapaswa kubadilika kidogo,ujuaji hauna nafasi kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad