Kimenuka..Wawili Wasimamishwa Kazi Tabora Sakala la Vichanga Kutolewa Macho"


Waziri wa TAMISEMI, Angellah J. Kairuki amesema amepokea kwa masikitiko malalamiko ya mzazi Kisaka Mtoisenga Mkazi wa
Ushikola wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Tabora, kufuatia Watoto wake mapacha waliozaliwa katika Kituo cha Afya Kaliua na baada ya muda mfupi kufariki na kukutana na dosari (wameng’olewa macho, kukatwa ulimi na kuchunwa ngozi kwenye paji la uso) baada ya Wazazi kukabidhiwa miili yao mnamo tarehe 10 Mei, 2023.

Kufuatia taarifa hiyo, TAMISEMI kupitia Halmashauri ya Wilaya ya
Kaliua imewasimamisha kazi Wauguzi wawili wa Kituo cha Afya Kaliua ili kupisha uchunguzi na imekabishi kwa Jeshi la Polisi suala hili ili waendelee na chunguzi wa tukio hili.

Kairuki amendelea kuwakumbusha Wataalam katika Vito vya kutolea huduma za Afya chini kote kuzingatia miongozo na taratibu za Kitaaluma zilizowekwa na Serikali wakati woe wanapohudumia Wananchi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad