Kipigo cha USMA, Kocha Nabi aitaja TFF, TPLB



Kocha Mkuu wa Klabu ya Young Africans Nasreddine Nabi, ametaja sababu ya kukosa ushindi kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Alger uliochezwa juzi Jumapili (Mei 28) Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.

Young Africans walichapwa mabao 1-2 na USM Alger na kuwaweka kwenye wakati mgumu wa kuchukua kombe hilo kwani wanatakiwa katika mchezo wa Mkondo wa Pili Juni 3, mwaka huu nchini Algeria, washinde kwa uwiano wa mabao 2-0.

Baada ya kipigo hicho, Nabi amesema hawakupata muda wa kutosha kujiandaa kama ambavyo ilitakiwa ndiyo maana wamepoteza.

Nabi amesema maandalizi hayakuwa bora sana kama ambavyo walitakiwa kuwa nayo kwa sababu walikuwa na muingiliano wa ratiba, hivyo muda mwingi walitumia kujiweka sawa.

“Maandalizi yetu ni magumu, hatujapata muda wa kutosha, tumetumia muda mwingi kwenye ‘recovery’, tunataka tutoe wito kwa wanaoandaa ratiba wafahamu tunaliwakilisha taifa, tunaombea siku zijazo lisitokee tena.

“Wachezaji walihitaji kuwa sawa na wakati wa kujiandaa hakuna namna nyingine, tunakaa na kuona tunachezaje mechi ya marudiano kwa sababu hata hivyo hatuna muda tena wa kutosha,” amesema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad