Aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Sunday Manara amesema kuwa jambo linaloiponza timu hiyo na kuishia robo fainali ya michuano ya CAF kila mwaka ni kujiona wao wakubwa kuliko timu nyingine hapa nchini na hata zile wanazokutaka nazo kimataifa.
Manara amesema hayo mara baada ya Yanga kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga Marumo Gallants ya Afrika Kusini huku Simba kwa miaka minne wakikomea robo fainali.
“Nilikuwepo Afrika kipindi kile nilipokuwa Kolo (Asante Mungu kunivua) tuliamini tunakwenda Semi final kirahisi Coz Kaizer Chiefs ilikuwa taabani.
“Maandalizi yetu yalikuwa ya hovyo, kambini kulijaa Confidence ya ajabu, matokeo yake kuingia uwanjani tukala ARBAA.
“Tofauti na huku Yanga, pamoja na Marumo kuwa hoi kwenye ligi ya kwao, hatukuwadharau na tulijua wanafanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho.
“Tulijua wanacheza ligi bora, tukaendelea kuwaheshimu hata baada ya kuwafunga mechi ya kwanza Dar, ugenini tukaja na plan ya kucheza kwa kuwaheshimu na kutumia counter attack, mwishoe tukatoboa.
“Mentalities za kujiona wakubwa na bora ndio zimefanya Makolo always waishie Robo fainali.
“Imagine unaenda kucheza na Kaizer unajiona wewe mkubwa zaidi yake, huku kwa Wananchi hakuna hivyo vitu, huku tunajua ili uwe mkubwa ni lazma ushinde mataji makubwa, sio kuishia robo robo kila siku,” amesema Manara.