Klabu ya Marumo Gallants imekanusha taarifa kuwa Wachezaji wao wamegoma kufanya mazoezi kuelekea mchezo wa Nusu Fainali mkondo wa pili Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga wakishinikiza kulipwa bonasi zao.
Tovuti ya FARPost iliripoti taarifa hiyo ambayo imechapishwa na mwandishi Ofhani Munyai mchana wa leo ikitaja sababu ni madai ya bonasi.
Taarifa ya Klabu muda mfupi uliopita inasema hakuna Mchezaji anayedai bonasi wala mshahara ni uzushi tu .