Kocha Nasreddine Nabi aishtukia Janja ya USMA , Hawa Lazima Tuwale Kichwa Kwao

Kocha Nasreddine Nabi aishtukia Janja ya USMA , Hawa Lazima Tuwale Kichwa Kwao
Kocha Nabi


Kocha wa Young Africans Nasreddine Nabi amesema ameshtukia baadhi ya mambo na anatarajia kubadili mfumo katika Mchezo wa Mkondo wa Pili wa Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USMA.


Baada ya juzi Jumapili (Mei 28) Young Africans kupoteza kwa kuchapwa 2-1, sasa wameanza mikakati ya mchezo wa Mkondo wa Pili utakayopiga Jumamosi (Juni 03) katika Uwanja wa Stade du 5 Juille.


Nabi amesema mchezo wa juzi Jumapili pale Uwanja wa Benjamin Mkapa aligundua ni wapi USM Alger waliwazidi ujanja.


“Yaliyotokea ni matokeo. Tulifanya baadhi ya makosa yaliyotufanya kupoteza mechi lakini bado tuna dakika 90 nyingine ugenini, na kuna mambo tumeshayagundua,” amesema.


“USM Alger ni timu bora na yenye wachezaji wachangamfu. Natambua ugumu wao hususan kwenye mechi ya ugenini lakini naamini tutajipanga upya na kwenda kutafuta matokeo mazuri kwao kwa kuwa tuna uwezo huo.”


Hata hivyo huenda Nabi akabadili mfumo na baadhi ya wachezaji katika kikosi alichokianzisha katika mchezo wa nyumbani Dar es salaam.


Young Africans inahitaji ushindi wa kuanzia mabao 2-0 ugenini ili kutwaa taji na kama itashinda 2-1 kama ilivyofungwa nyumbani basi mchezo utamaamuliwa kwa mikwaju ya Penati.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad