Mitandao mbalimbali ya Habari za michezo Ulaya imeripoti kuwa Club ya Paris Saint-Germain (PSG) imeamua kumsimamisha kazi kwa wiki mbili Mchezaji wake Lionel Messi kutokana na kusafiri kwenda Saudi Arabia wiki hii bila ruhusa ya Club.
PSG imeripotiwa kumsimamisha Messi kwa wiki mbili bila malipo baada ya kutohudhuria mazoezi bila kibali na kusafiri kwenda Saudi Arabia ambako alipigwa picha akiwa kwenye Mji wa Riyadh siku ya Jumatatu. #MillardAyoSPORTS