Mchezaji wa Real Madrid Vinicius Junior amesema "La Liga ni ya wabaguzi wa rangi" baada ya kushambuliwa kwa maneno ya kibaguzi huko Valencia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifukuzwa kazi kwa kufanya vurugu kwa dakika 97 baada ya kuzozana na Hugo Duro.
Mapema katika mchezo huo, Vinicius aliyepandwa nahasira alijaribu kumfahamisha mwamuzi kuhusu vitendo vya shabiki wa Valencia.
“Michuano ambayo hapo awali ilikuwa ya Ronaldinho, Ronaldo, Cristiano na Messi leo ni ya wabaguzi wa rangi,” aliandika kwenye Instagram.
"Haikuwa mara ya kwanza, wala ya pili, wala ya tatu. Ubaguzi wa rangi ni jambo la kawaida kwenye La Liga. Wasimamizi wa mashindano hayo wanafikiri ni jambo la kawaida, Shirikisho na wapinzani pia wanaendekeza suala hili.
"Taifa zuri, ambalo lilinikaribisha na ninalipenda, lakini limekubali kuonekana kama nchi ya kibaguzi duniani. Samahani kwa Wahispania ambao hawakubalian na mimi, lakini leo hii huko Brazil, Uhispania inajulikana kama nchi ya wabaguzi.
"Na kwa bahati mbaya, kwa kila kitu kinachotokea kila wiki, sina utetezi. Ninakubali. Lakini nina nguvu na nitaenda hadi mwisho kupaza sauti dhidi ya wabaguzi. Hata kama ni mbali na hapa."
Katika taarifa yake, La Liga ilisema imekuwa "ikipigana na aina hii ya tabia kwa miaka mingi, pamoja na kukuza maadili chanya ya michezo, sio tu kwenye uwanja wa uchezaji, lakini pia nje ya mchezo".