Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ametoa maelezo kwenye mitandao yake ya Kijamii kuhusu tetesi za uwepo wa COVID-19 nchini Tanzania, ameandika;
“Kuhusu tetesi za uwepo wa #COVID19; Nawaomba wananchi muondoe hofu. Tunachakata taarifa tulizokusanywa kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii...tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au la??
Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya UVIKO-19 wiki tarehe 6 - 12 Mei 2023 Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona. Hii ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya tarehe 29/04/23 hadi 05/05/23. Hakuna kifo chochote kilicho thibitishwa kusababishwa na UVIKO-19. Wizara @wizara_afyatz inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili. Nawaomba wananchi muendelee kuzingatia kanuni za Afya na Usafi.”