Mahakama Yaungua Moto, Nyaraka Zote za Kesi zateketea


Mahakama ya Mwanzo Shanwe iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi imeungua moto na nyaraka zote zilizokuwemo ndani yake kuteketea baada ya moto kuwaka Mahakamani hapo usiku wa kuamkia leo.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa huo Regina Kaombwe amesema taarifa za jengo la Mahakama hiyo kuungua moto walizipata saa sita na robo usiku baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali mtaa wa Shanwe, Mustapha Kimasa.

Kaombwe amesema majira ya saa sita na dakika ishirini na saba Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo la tukio na kufanya juhudi za kuuzima moto uliokuwa tayari umeshasambaa jengo lote la Mahakama.

Hata hivyo amesema moja ya changamoto waliyokabiliana nayo ni baada ya maji kuisha walilazimika kuwagongea wananchi wanaokaa jirani na jengo la Mahakama hiyo ili watoe msaada wa maji ambao walijitolea ndoo za maji na kuanza kushirikiana na Jeshi hilo kuuzima.

"Wakati tunaendelea kuzima moto mlinzi wa Mahakama hakuwepo katika kituo chake cha kazi, wakati gari la Zimamoto lilipoishiwa maji walielekea kwenye hiderent zote tatu mjini hapa na wakakosa maji"

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema dalili zinaonyesha kuna hujuma zimefanyika hivyo anaunda timu itakayochunguza chanzo cha moto huo ndani ya siku tano kisha watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad