Majaliwa aipongeza Yanga, aitaka Simba ijifunze




WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kuichabanga timu ya Marumo Galants kutoka nchini Afrika Kusini jumla ya bao 2-0 na kuweka matumaini ya kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la shirikisho barani Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Mei 2023 bungeni jijini Dodoma ambapo mbali na kuipongeza amesema wawakilishi hao pekee wa Tanzania, wanaipeperusha bendera ya Taifa vizuri.

“Tunawaombea sana washinde kwa magoli mengi kwani Watanzania tunahamu ya kuona klabu ya Tanzania ikiingia hatua ya fainali.

“Pia niipongeze Simba SC. kwa hatua waliyofikia, tunaamini wamejifunza na kuona kutoka kwa klabu jirani. Tunaamini katika msimu ujao kwenye mashindano hayo tutaingiza klabu mbili au zaidi,” amesema.


Baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali uliopigwa jana tarehe 10 Mei 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga inatarajiwa kurudiana katika mechi ya mkondo wa pili tarehe 17 Mei 2023 nchini Afrika Kusini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad