Makonda, Lemutuz wafutiwa kesi




MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imefuta kesi ya madai ya gari, iliyofunguliwa na mfanyabiashara, Patrick Kamwelwe (PCK) dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na William Malecela (Le Mutuz) kufuatia mdai kutoonekana mahakamani.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabate aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo baada ya mawakili wa utetezi Gift Joshua na Simon Mawala kuwasilisha ombi la kufuta kesi hiyo mahakamani hapo kwa sababu shauri hilo limekuwa likiahirishwa mara kwa mara.

Mheshimiwa Hakimu hii ni mara ya nne mfululizo mdai pamoja na mawakili wake wamekuwa hawajatokea mahakamani, tunaomba shauri hili lifutwe" amedai wakili anayemuwakilisha Makonda katika kesi hiyo, Gift Joshua.

Hakimu Kabate alikubali ombi hilo la utetezi na kufuta kesi hiyo.

Katika kesi ya msingi, Kamwelwe anadai yeye alikuwa anamiliki gari aina ya Range lover ambapo kutokana na urafiki wake na Lemutuz na urafiki kati ya Lemutuz na Makonda ndio Makonda aliomba kuitumia ile gari .


Anadai Yeye alimkabidhi Lemutuz gari hiyo ili ampatie Makonda aweze kuitumia wakati alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kwamba katika makubaliano yao ilikuwa ni kwamba angeitumia gari hiyo kwa kipindi cha wiki mbili kisha angeirudisha lakini haikuwa kama waliyokuwa wamekubaliana, baada ya wiki mbili kukamilika bado Makonda aliendelea kuitumia hiyo gari na mpaka leo hajarejeshewa gari yake.

Pamoja na mambo mengine mdai anaiomba mahakama kurejeshewa thamani halisi ya kiasi cha pesa alichotumia kununulia hiyo gari, anadai pesa ya usumbufu, garama za kutokuwa na gari yake kwa kipindi chote hicho.

Pia, Kamwelwe anaiomba mahakama imuamuru Makonda na mwenzake, kumlipa kiasi hicho cha fedha kama fidia anayodai kuwa, imetokana na hatua ya wadaiwa hao kumdhulumu gari lake jeusi aina ya Toyota Rand Rover/Range Rover Ronge Sport, yenye namba 20153.


Katika mchanganuo wa fedha hizo, Sh. 247,243,750, ambazo ni sawa na dola za Marekani 106,250, Kamwelwe anamtaka Makonda na mwenzake, walimpe dola 11,250, kama gharama ya kodi ya kuliingiza gari hilo. Dola 50,000, fidia ya kutwaa gari, pamoja na dola 45,000, ambayo ni thamani ya gari
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad