Marekani Yakanusha Kupanga Shambulio La Droni La Moscow

 


Msemaji wa Usalama wa taifa nchini Marekani John Kirby.

Marekani imekanusha madai kwamba ilipanga shambulio la ndege isiyokuwa na rubani inayodaiwa kuishambulia Kremlin siku ya Jumatano kwa lengo la kumuua Rais Vradimir Putin.


Siku moja baada ya kuishutumu Ukraine kwa kutekeleza shambulio hilo, msemaji wa Bw Putin amesema lilifanywa kwa usaidizi wa Washington.


Msemaji wa Usalama wa taifa nchini Marekani John Kirby ameyaita “madai ya kejeli”.


Ukraine imesema haihusiki na shambulio linalodaiwa. Bw Putin hakuwepo katika katika jengo la Kremlin wakati huo.


Ukraine imeishutumu Moscow kupanga tukio hilo ili kuendeleza vita zaidi.


Licha ya kwamba mashambulio ya Urusi yameendelea bilakupungua – watu 21 waliuawa Jumatanokatika jimbo la Kherson lililopo kusini mwa Ukraine – bado hakuna dalili kwa upande wa Urusi ya kufanya mashambulizi makali.


Jumapili jioni ndege isiyokuwa na rubani ilidunguliwa katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, katika eneo ambalo sio mbali sana na ofisi ya rais.


Maafisa baadaye walikiri kuwa ilikuwa ni droni ya Ukraine ambayo ilikuwa “imepoteza udhibiti” na kwamba iliharibiwa ili kuepusha “athari mbaya”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad