Marumo Gallants wagomea mazoezi kisa bonasi





Wachezaji wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini wamegoma kufanya mazoezi mchana huu kwa sababu hawajapata bonasi waliyoahidiwa.

Timu hiyo kesho itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Royal Bafokeng saa 12 jioni kwa muda wa Afrika Kusini sawa na saa 1 usiku Tanzania.

Chanzo cha wachezaji hao kugoma na kukaa hotelini walipoweka kambi ni kutopata bonasi ambayo waliahidiwa na uongozi wakivuka nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu wa jarida la FARPost wachezaji hao si mara ya kwanza kufanya hivyo kwani mechi ya robo fainali dhidi ya Pyramids FC walitishia kugoma ila baada ya mazungumzo walikubali kuingia uwanjani.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad