Maskini Paul Pogba Atokwa na Machozi ya Damu Baada ya Kuumia Tena, Atoka nje ya Uwanja

Paul Pogba
Paul Pogba

Nyota wa Juventus Paul Pogba alijikuta akiangusha machozi baada ya kupata jeraha lililomlazimisha kutoka nje wakati mchezo wao dhidi ya Cremonense ukiendelea.

Kiungo huyo wa Ufaransa amejikuta kwenye wakati mgumu huko Juventus baada ya kujiunga tena na waajiri wake wa zamani. Paul Pogba amehusika kwenye mechi kumi pekee katika michuano yote tangu arejee kutoka Manchester United kutokana na matatizo ya majeraha.

Pogba alionekana kuwa fiti alipoanza katika pambano la Serie A dhidi ya Cremonese kwenye Uwanja wa Allianz. Hata hivyo, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alipata jeraha lingine baada ya dakika 24 tu na ikabidi atolewe nje na meneja wa Juventus Massimiliano Allegri.

Kiungo huyo mwenye miaka 30 aligubikwa na machozi wakati akitoka uwanjani na kutumia jezi yake kufunika uso huku nafasi yake ikichukuliwa na Arkadiusz Milik.

Pogba huenda asionekane tena msimu huu, wakati Juve wamebakiwa na mechi tatu za Serie A pamoja na ratiba ya Ligi ya Europa

Pogba atalazimika kuelekeza nguvu zake kwenye kurejea katika utimamu kamili wa mwili kwa wakati kwa ya ajili ya msimu wa mwaka 2023-24

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad