Maswali Magumu Kwa Eng Hersi wa Yanga na TFF Kuhusu Sakata la Fei Toto..Kumekucha




Anaandika @scanda24 ✍️

'📌Eng Hersi anasema Yanga ni Taasisi inayofuata misingi ya Taasisi na wala haina huruma, iweje iendelee kumlipa mtumishi aliyetoroka kwa miezi mitano.? Taasisi yoyote yenye misingi haiwezi kufanya wanachofanya Yanga, aseme Ukweli nini kimejificha nyuma ya Fei Toto na Yanga'

'📌Eng Hersi anasema Fei Aidha auzwe, aboreshewe maslahi au arudi atumikie mkataba wake hadi 2024. Ukiona anavyoongea unaona kabisa wanajificha kwenye kivuli cha upendeleo wa TFF kwamba ni haramu kuvunja mkataba'

📌Eng Hersi anajua kabisa kuwa mchezaji anaweza kuondoka bila kutakiwa na timu yoyote, anaweza kuondoka kabla ya muda wa mkataba kuisha na mkataba unaweza kusitishwa muda wowote. Kinachofanyika ni Kuwahadaa MAZUMBUKUKU.
.
📌Kisha anasema katika makubaliano ya kimkataba wenyewe wanatimiza jukumu lao kwa Fei. Jiulize, kama Taasisi inamlipa mchezaji ili acheze, huu mwezi wa Tano Feisal hatimizi jukumu, kwa nini hawachukui hatua.? Aseme Ukweli, Misingi ya Taasisi haipo hivyo.
.
📌Kusema Kamati imesema kuwa Feisal hana haki ya kuvunja mkataba ni kukiuka sheria za FIFA ibara ya 17 (upande wowote unaweza kuvunja mkataba) inayosema mkataba unaweza kuvunjika kwa Gharama za uvunjaji wa bila makubaliano (FIDIA).
.
📌Kamati ya hadhi na sheria za wachezaji ya TFF kwa namna alivyoongea wamejivua nguo wote, Hakuna Mkataba usiweza kuvunjika. Pia anasema wazi, hakukua na wanasheria upande wa Fei wakati wa kusaini mkataba. Je, Tuuite huu ni Ulaghai?

By Scanda24

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad