Membe "amtoa" Chozi Kikwete

 


Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akiaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe

Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete akiaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe

Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe.


Membe aliyehudumu kama Naibu waziri na waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne alifariki dunia Mei 12, 2023 na anatarajiwa kuzikwa Mei 16 mwaka huu katika, Rondo mkoani Lindi.


Kikwete ambaye alikuwa safarini nje ya nchi amewasili saa 8:28 mchana ikiwa ni dakika kadhaa baada ya viongozi wengine wa kitaifa kuondoka viwanjani hapo.


Moja kwa moja baada ya kuwasili Kikwete alielekea kwenye eneo lililowekwa kitabu cha kuandika salamu za pole kisha kuelekea walipokaa wanafamilia.


Kikwete akiwa mwenye huzuni aliwasalimia wanafamilia kisha kupita pembeni ya jeneza la Membe, uso wake uliongezeka simanzi alipomuona waziri wake huyo wa zamani ndani ya jeneza.


Ilimlazimu Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kumshika mkono kiongozi huyo mstaafu wakati akishika ngazi baada ya kuaga mwili wa mwanadiplomasia mahiri nchini.


Punde baada ya kumaliza kuaga Kikwete aliingia kwenye gari yake na kuondoka viwanjani hapo.


Kikwete ndiye aliyemteua Membe kuwa Naibu waziri wa mambo ya ndani kisha Naibu Waziri wa Nishati na Madini na mwaka 2007 akamteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad