Mkaliwenu Amchapa Yusuph Mlela Katika Pambano la Ngumi



Mchekeshaji Mkaliwenu amemshinda Mwigizaji Yusuph Mlela kwenye pambano lao lililofanyika usiku wa kuamkia leo ikiwa ni pambano la utangulizi kusindikiza pambano kuu katika viwanja vya FayHeroes Martial Art Club Mikocheni Jijini Dar es salaam.


Mkaliwenu alitangazwa Mshindi baada ya kumshinda Mpinzani wake kwa points ambapo baada ya pambano hilo Mlela amesema;


“Ni kawaida kwa sababu kwenye mchezo wa ngumi kuna kupoteza, kikubwa ni kwamba mimi nimemfata kwenye mchezo wake Mkaliwenu anafanya kick boxing kwa hiyo nilifanya mazoezi ya kick boxing kwa kipindi kifupi.


“Mara nyingi alikua akicheza faulu na kupiga mateke ya sehemu za siri, nitajipanga wakati mwingine na kumuomba turudiane ili tufanye boxing,” amesema Yusuph Mlela.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad