Mkanganyiko kujiuzulu kwa Meja Jenerali Nyagaya




Jumuiya ya Afrika Mashariki – EAC, inasema barua ya kujiuzulu  ya Kamanda wa kikosi cha Jeshi cha Jumuiya hiyo, Meja Jenerali Jeff Nyagah inayosambaa mtandaoni haina uhalali. 

Taarifa ya EAC, imekuja baada ya Jeshi la Kenya pia kutoa taarifa mfanano kuwa Kamanda huyo hakujiuzulu kama inavyoelezwa kwamba alikuwa akihofia usalama wake kutokana na kampeni chafu za vyombo vya habari nchini DRC juu ya operesheni za kikosi hicho na kukwamisha utendaji wake. 


Hata hivyo, Meja Jenerali Nyagah, alithibitisha kuondoka kwake nchini DRC wakati akihojiwa na chombo kimoja cha Habari, na kusema alikuwa amerejea Nairobi kwa mashauriano, ambako ameteuliwa kwenye nafasi nyingine katika jeshi la Kenya. 

Ripoti za ndani za kidiplomasia na zile za kutoka katika serikali ya DRC, zimethibitisha uhalali wa barua hiyo, na ikumbukwe kuwa Kikosi cha Jeshi la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, kinaundwa na mataifa saba ili kusaidia kuleta utulivu Mashariki mwa DRC na kupambana na makundi ya waasi. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad