Nairobi. Polisi nchini Kenya, wamemkamata mke wa Mchungaji, Paul Mackenzie kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea dhidi ya Kanisa la Good News International Church ambalo waumini wake walishawishiwa kufa kwa njaa ili waende mbinguni.
Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Nation la Kenya, Mke wa Mhubiri huyo Rhoda Maweu, alinaswa kutoka mafichoni huko Mtwapa katika Kaunti ya Kilifi pamoja na shangazi yake jana Jumatatu usiku.
Chanzo cha kuaminikia ndani ya Jeshi hilo ambacho kinachohusika na uchunguzi huo, kimeaimbia Nation kuwa Mwaweu imetambuliwa kama mhusika mkuu katika shughuli za kanisa hilo.
Mhubiri Mackenzie ameshutumiwa kwa kuwahadaa watu kupitia mafundisho potofu, yaliyojaa hofu kwa watu katika kuutafuta wokovu, na hivyo kusababisha vifo vya wengi.
Kiongozi huyo aliyejifanya kuwa kiongozi wa kiroho yuko chini ya ulinzi wa polisi kwa madai ya kuhubiri fundisho hatari linalowahimiza wafuasi wake kujiua kwa njaa ili waende mbinguni.
Kama sehemu ya uchunguzi, polisi wamekuwa wakipitia rekodi za simu za mkononi za Mackenzie na kuwahoji watu wanaofungamanishwa na dhehebu hilo.
Jina la Mwaweu limetajwa kuwa na umuhimu kutokana na majukumu yake kama meneja rasilimali watu wa dhehebu hilo ambapo Polisi wanachunguza hayo majukumu yake.
Wachunguzi hao wanaamini kwamba alikuwa mtu muhimu katika usimamizi wa kanisa na alichangia katika mafundisho ya kanisa yenye kutiliwa shaka ambayo kimsingi yamesababisha vifo vya watu kadhaa.
Inasemekana kuwa Polisi wamepekua rekodi za simu za Mackenzie na kugundua jumbe kadhaa za mashtaka kati yake na mkewe.
Polisi wanasema Mwaweu ilichukua jukumu muhimu katika kusajili waumini wapya katika dhehebu hilo. Pia inadaiwa kuwa huenda alipata taarifa nyeti za kifedha na huenda alihusika katika kufanya maamuzi ya kifedha kwa niaba ya dhehebu hilo.
Mumbua ni mke wa tatu wa Mackenzie. Mke wa kwanza wa Mackenzie alikufa mnamo 2009 na kuacha watoto wawili.
Mnamo 2012, alioa tena na mkewe alikufa mnamo 2017 na kuacha watoto wanne. Mackenzie alimuoa Mumbua mara tu baada ya kifo cha mke wake wa pili.