Msako biashara ya maua yaliyoibwa makaburini waanza



Polisi katika jiji la Ankara nchini Uturuki, wameanza upelelzi katika maduka ya kuuza maua ya ndani ya jiji hilo, ili kuwakamata wauza maua wanaouzia watu maua yaliyoibwa makaburini.

Upelelzi huo wa Polisi, unafuatia ripoti za raia wema katika vituo vya polisi wakilalamikia kuibwa kwa maua na mapambo mengine ikiwemo mishumaa ya thamani katika makaburi ya wapendwa wao.


Polisi wanasema, wizi huo unatokana na watu wengi kukosa fedha za kununulia maua na mapambo mapya katika maduka, na hivyo kulazimika kununua maua yaliyokaa dukani kwa juma moja au zaidi.

Hatua hiyo imesababisha wezi huvamia makaburini na kuiba maua na kwenda kuyauza katika mduka hayo, jambo lililowafanya Polisi kutaka kubaini maduka yanayoshawishi wezi kuiba maua makaburini na kisha kuyanunua ili kuyauza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad