Msanii Nini Achafua Hali ya HEWA "Huwezi Kufanya Kolabo na Msanii wa Kiume Bila Kukuomba Rushwa ya Ngono"

 


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nini ambaye alikuwa chini ya lebo ya Free Nation inayomilikiwa na msanii Nay wa Mitego amefunguka kuwa anachukizwa na vitendo vinavyoendelea kwenye muziki wa Bongo Fleva.


Nini amesema hilo linatokana na ukweli kuwa mambo wanayoyapitia wasanii wengi wa kike ni aibu na yanakatisha tamaa kuendelea na shughuli za muziki hivyo anaona ni bora kuachana na muziki na akafanya shughuli nyingine.


"Jamani huu muziki Wa Bongo Fleva ulipofikia si pazuri sana hasa kwa sisi wasanii wa kike. Kuna muda natamani kuacha muziki kabisa.


"Yani huwezi kufanya kolabo na msanii wa kiume bila kukuomba rushwa ya ngono, nimechoka sasa na bila mapenzi ningekua mbali sana kimuziki yamechangia kushuka kwangu kwenye ubora wa muziki," ameongea Nini

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad