Hatimaye Msanii nguli wa Tanzania Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay amerudi tena kwenye mitandao ya kijamii kwa mara ya kwanza leo ikiwa ni baada ya siku zaidi ya 462 za kutokuweka chochote kwenye kurasa zake baada ya kuugua na kulazwa Hospitali ambapo kwenye post yake leo ameweka picha ya muonekano wake wa sasa aliyoipiga leo.
Profesa Jay ameanza kwa kuandika "Salaam Ndugu zangu, kwanza namshukuru sana MUNGU aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu), pili kipekee namshukuru sana Mhe. Rais Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi, Asante sana Mama pamoja na Serikali yako yote kwani Viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji"
"Tatu namshukuru sana Mwenyekiti wa Chama changu cha CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe, Wanachama na Viongozi wote waandamizi wa Chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na Serikali, zaidi nawashukuru sana Madaktari na Manesi wote wa Muhimbili kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu AHSANTENI SANA"
Mkali huyu wa Bongofleva pia alimalizia kwa kuwashukuru Watanzania wote waliojitolea kwa maombi na pesa ambazo zilimsaidia sana kulipia gharama za awali kabla ya Serikali kuingilia kati na kusema itagharamia kila kitu, Watanzania mbalimbali aliowashukuru Profesa Jay ni pamoja na Malisa GJ, Iyenda, Vyombo vyote vya habari na social media kama Clouds FM, Millard Ayo, Wasafi FM, Watumishi wa Mungu kama Wachungaji, Mashekh na Mapadre, Familia yake akiwemo Mke wake, Kaka zake, Dada zake, Wadogo zake na Familia yote ya Mzee Haule.
"Kwa sasa nipo imara na ninaendelea vizuri sana Mungu ni mwema sana siku zote🙏🏻🙏🏻🙏🏻,Ahsanteni…… Joseph Haule (Prof. Jay) #MgodiUnaotembea #SeeYouSoonm127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa0 " ——— amemalizia kwa kuandika @ProfessorJayTZ