Mwamba Aliyeingia Chumbani Kwa Malkia Elizabeth Baada ya Kuruka Ukuta wa Ikulu...Inatisha




Imekuwa kawaida kwa binadamu kujaribu mambo mbalimbali hata yale ambayo wengine huamini kuwa ni ngumu kufanyika, mwaka 1982, mwanaume aliyefahamika kwa jina la Michael Fagan alifanikiwa kuruka ukuta mrefu wa Ikulu ya Buckingham, na kuingia hadi katika chumba cha Malkia Elizabeth II bila ya walinzi kumuona waliokuwa wamebeba silaha kali.

Michael Fagan aliruka ukuta huo wa Buckingham Palace wenye urefu wa mita 4.3 huku juu ukuwa na senyenge zenye miiba bila ya kuhofia kitu inaelezwa kuwa baada ya kuruka ukuta alipitia dirishani na aliingia ndani ya jumba hilo, na kuzunguka kwa dakika 30 kabla ya kuzama kwenye chumba cha #Malkia kisha mida ya saa 7.15 asubuhi aliingia kwenye chumba cha kulala cha Malkia.

Dakika hizo 30 kabla ya kuingia katika chumba cha malkia alizitumia kushangaa mandhari nzuri ya jengo hilo, akaingia kwenye ofisi ya malkia na kukaa kwenye kiti cha enzi akipumzika huku akinywa mvinyo mweupe wa malkia aliyoukuta katika ofisi hiyo. Baada ya kumaliza mvinyo ndipo aliamua kuzama kwenye chumba cha malkia ambapo alimkuta kalala.

Michael alikaa kimya pembeni ya Kitanda hadi muda ambao #Malkia alishituka na kukutana na sura ngeni asiyoielewa ikapelekea kupiga kelele zilizofanya walinzi wafike na kumkamata jamaa kwa kumuweka chini ya ulizi. Michael alishtakiwa kwa kosa moja tu la kuiba mvinyo mweupe wa malkia na kunywa, shitaka ambalo baadaye lilitupiliwa mbali huku Mahakama ikaamuru afanyiwe vipimo vya akili, baadaye aliachiwa huru huku baadhi ya #Askari walifukuzwa kazi kutokana na uzembe .

Michael Fagan alizaliwa #Clerkenwell, London mwaka 1948 na mwaka 1966 akiwa na umri wa mika 18 alimkimbia baba yake na kwenda kutafuta maisha yake kwa kudai kuwa baba yake ni mkali

Imeandikwa na @officialtinana

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad