Nchi 10 zinazoongoza kwa talaka duniani




Viwango vya talaka vinatofautiana kote ulimwenguni, huku nchi fulani zinakabiliwa na viwango vya juu zaidi kuliko nchi nyingine.

Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za dunia za nchi kama vile Marekani na Canada, takriban asilimia 40% ya ndoa zote huishia kwenye talaka; huku Japan, kiwango ni 1.2% tu.

Ukiacha hizo zipo nyingi tu na zipo sababu kadhaa zinazotajwa kuchangia talaka ikiwemo.

Mgogoro wa kifedha
Tabia tofauti
Uraibu
Utamaduni tofauti
Kunyimwa unyumba
Kudanganya
Tofauti za kidini na mengine

Lakini hapa tunakuletea nchi 10 ambazo watu wake wanapeana talaka nyingi zaidi ulimwenguni.


10. Costa Rica

Costa Rica ni taifa linalozungukwa na milima, misitu na bahari huko Amerika. Ikiwa na watu 5.1milioni yenyewe inashika nafasi ya 10 kwa viwango vya talaka duniani. Ina wastani wa asilimia 2.8 ya talaka kwa kila watu 1,000.

9. Ukraine

Ukraine inapitia kipindi kigumu cha vita dhidi ya Urusi. Ni mwaka sasa na miezi karibu mitatu inakwenda minne tangu Urusi iivamie nchi hiyo jirani yenye watu 43.milioni.

8. Georgia

Georgia yenye watu 3.7milioni inashika nafasi ya nane duniani kwa wastani wa asilimia 2.9% ya talaka katika kila watu 1,000.

7: Aruba

Aruba, ni nchi inayounda Ufalme wa Uholanzi iliyoko kusini mwa Bahari ya Caribbean. Ni kama kilomita 29 kaskazini mwa peninsula ya Venezuela ya Paraguaná na kilomita 80 kaskazini-magharibi mwa Curacao. Yenyewe inashika nafasi ya saba kwa talaka. Asilimia 2.9% katika kila watu 1,000.

6: China

Taifa lenye watu wengi wapatao 1.4 bilioni. Lenyewe pia linakumbana na mizozo ya talaka na kwa mujibu wa takwimu ina wastani wa asilimia 3.2% ya talaka katika kila watu 1,000.

5: Belarus

Belarus taifa lingine dogo lenye idadi kubwa ya talaka duniani. Kwa mujibu wa takwimu linashika nafasi ya tano ikiwa na wastani wa asilimia 3.7% ya talaka kwa kila watu 1,000.

4. Moldova

Moldova, ni moja ya nchi ndogo Mashariki mwa Ulaya ambapo zamani ilikuwa chini ya Umoja wa Soviet. Ikizungukwa na milima ina watu 2.6mil ikishika nafasi ya nne kwa asilimia 3.8 ya wastani wa talaka.

3: Urusi


Urusi inashika nafasi ya nne kwa talaka nyingi duniani. Moja ya mataifa makubwa na yenye idadi kubwa ya watu ambapo ina wastani wa asilimia 3.9% ya takala kwa kila watu 1,000.

2. Kisiwa cha Guam

Kisiwa hiki kinashika nafasi ya pili kwa talaka nyingi kikiwa na wastani wa talaka wa asilimia 4.3 kwa kila watu elfu moja.

1: Maldives

Kwa upande wa idadi ya talaka katika nchi hii kwa 2023, iko katika nafasi ya kwanza duniani ambapo kuna talaka 5.5 kwa kila watu 1000 talaka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad