Paula Kajala "Niko tayari kuolewa na Marioo"

Paula Kajala "Niko tayari kuolewa na Marioo"


Mwanamitindo wa Tanzania, Paul Paul Kajala ameeleza imani yake kwamba mwimbaji Omary Mwanga almaarufu Marioo atamfanya mkewe.


Katika video inayosambaa mitandaoni, binti huyo wa muigizaji Kajala Masanja anasikika akisema kwa ujasiri kuwa yeye ni mpenzi wa Marioo.


"Wewe ni demu wa nani?" mwanamume ambaye alikuwa akimrekodi alisikika akimuuliza kwenye video hiyo.


Paula kwa madaha ya alijibu, "Omary!"


Mwanamume huyo aliendelea kumuuliza mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20 kama Marioo ana mpango wa kumuoa siku moja.


"Kwa nini isiwe hivyo?" Paula alijibu kwa sauti ya kijasiri.


Takriban wiki mbili zilizopita, Paula Kajala kwa hasira nyingi aliwasuta watu wanaoingilia maisha yake hasa ya mahusiano.


"Ifike mahala mheshimu maisha ya mtu binafsi, nina haki ya kuwa na mtu nimpendaye kama watoto zenu/ndugu zenu/na nyinyi wenyewe mnavyofanya (Tofauti yetu, nyinyi mnafanya gizani mimi ninawaonyesha)," alisema.


Binti huyo wa muigizaji wa filamu bongo Frida Kajala Masanja aliwataka wanaoingilia mahusiano yake kukoma huku akibainisha kwamba wengi wao ni wanawake wakubwa wanaostahiki kuwa mamake.


Alihoji jinsi wakosoaji wake wanataka aishi maisha yake kuona kwamba baadhi yao wanapinga hatua zake.


"Wengi ni mama zangu mnaoongea kwa hasira vitu ambavyo siyo vya ukweli. Natumia lugha nyepesi sana, achaneni na maisha yangu.


Nilimpenda wa kwanza nikamtambulisha tukaachana, mlikuwa mnatakaje? Nisidate tena? Au nisidate kisirisiri?," alihoji.


Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20 aliwataka wakosoaji kuangazia familia zao na kutoingia maisha yake.


"Mungu tu anaweza kunihukumu! Nyie waungu watu wa kwenye mitandao muda huu mngeutumia kuabudu makanisani/ msikitini na mngekuwa mmekokoa roho za watu wengi kuliko hichi mnachokifanya. Nimewachoka," alisema.


Paula alidokeza kuwa baadhi ya wakosoaji walitaka kumuona amehuzunika baada ya kuachana na Rayvanny mwaka jana. Aliendelea kubainisha kwamba anamshukuru Mola kwa kumbariki na kumbariki na bavu lake, Marioo.


"Mniache niishi kwa amani mnitoe kwenye midomo yenu hata nikiharikiwa nyie inawahusu nini kwa sababu hakuna ata mmoja anayenisaidia mpaka hapa nilipo. Achaneni na mimi mfocus na maisha yenu. Maisha yangu yatawasumbua na hakuna cha maana mtakachokipata kwa kuniongelea mimi vibaya," alisema.


Paula alimtambulisha Marioo kama mpenzi wake mpya siku chache tu baada ya aliyekuwa mpenziwe, Rayvanny kuthibitisha kufufuka kwa mahusiano yake na mzazi mwenzake Fahyma almaarufu Fayvanny.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad