Chuma kimegonga miaka 98 leo. Katika maisha yake Mungu amempa neema ya uongozi, umri, hekima na afya. Pamoja na umri huu mkubwa macho yake bado yanafanya kazi vizuri bila msaada wa miwani. Hii ni neema ya ajabu maana siku hizi tuna vijana wadogo bila miwani hawawezi kujiona hata wao wenyewe 🤣.
Katika umri huu mkubwa bado ana uwezo wa kutembelea bila msaada wa fimbo. Alipofikisha miaka 94 yalifanyika matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangia wagonjwa wa moyo. Yalikua matembezi ya kilomita 5. Mzee Mwinyi aliwazidi vijana wengi ambao walipotembea kilomita moja walianza kusikia harufu ya maini na mapafu yao yakijikaanga, hivyo wakalzimika kudandia bodaboda ili iwapige tafu 🤣.
Pamoja na kwamba kuishi kwetu ni kwa neema ya Mungu tu (Filipi 1:21), lakini siri nyingine mzee Mwinyi ni mtu wa sala sana (soma kitabu cha maisha yake utaelewa). Pia ni mtu wa haki. Kwenye uongozi wake kama Rais aliwatendea haki hata wale waliomdhulumu akiwa hana madaraka. Mnakumbuka kisa cha yule Waziri aliyemtimua kwenye nyumba, halafu Mwinyi alipokuja kuwa Rais, wala hakulipiza kisasi, bali alimteua tena kuwa Waziri.
Lakini siri nyingine ya mafanikio, hii alinidokeza kaka @kitilamkumbo ni kwamba Mzee Mwinyi ana wake wawili. Inadaiwa watu wenye wake wawili huishi muda mrefu kuliko wenye mke mmoja. Hili itabidi tulifanyie research kama ni kweli tudai Katiba mpya kwenye makanisa yetu. Naam, Katiba mpya ni sasa (jokes 🤣). Happy birthday mzee Ruksa. Tunamtukuza Mungu kwa maisha yako.!