Rais Samia awapa ujumbe watahiniwa kidato cha sita



Wanafunzi wakifanya mtihani
RAIS Samia Suluhu Hassan, amewataka kheri watahiniwa wa mtihani wa kumaliza kidato cha sita, huku akiwaahidi kwamba Serikali yake inaandaa mazingira Bora ya hatua zinazofusta ikiwemo vyuo vya ufundi, vya kati na elimu ya juu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa ujumbe huo Jana Jumatatu, kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo wahitimu hao wanatarajiwa kuanza mitihani kuanzia Leo tarehe 2 Mei 2023, Hadi mwishoni mwa mwezi huu.

Nawatakia kila la kheri wanangu wote mnaoanza mitihani yenu ya Kidato cha Sita kesho. Tunawategemea. Tunawaamini.

Nawatakia kila la kheri wanangu wote mnaoanza mitihani yenu ya Kidato cha Sita kesho. Tunawategemea. Tunawaamini.


Naamini mmejiandaa vyema kwa hatua hii muhimu kwenye safari yenu ya elimu, na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape utulivu na siha njema mkahitimishe salama na kwa…

— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) May 1, 2023

“Naamini mmejiandaa vyema kwa hatua hii muhimu kwenye safari yenu ya elimu, na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape utulivu na siha njema mkahitimishe salama na kwa mafanikio,” ameandika Rais Samia na kuongeza:


“Serikali itaendelea kuhakikisha inaandaa mazingira bora katika safari yenu kuelekea hatua zifuatazo ikiwemo Vyuo vya Ufundi, Vyuo vya Kati na Vyuo vya Elimu ya Juu.”

Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), jumla ya watahiniwa 106,956, wamesajiliwa kufanya mtihani wa mwisho wa kumaliza kidato cha sita, kuhu watahiniwa 8,906 wakisajikiwa kufanya mitihani ya mwisho ya kozi ya ualimu katika ngazi ya astashahada na cheti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad