Rick Ross kufanya ngoma na Navy Kenzo



Rapa kutoka nchini Marekani Rick Ross akiwa IG live na kundi la muziki Bongo la Navy Kenzo usiku wa kuamkia leo ameonesha kuikubali ngoma yao ya Sip & Whine.

Rick Ross amesikika akisema kwamba atafurahi verse yake ikiwepo kwenye remix ya ngoma hiyo kwani ameikubali sana kutokana na vibe iliyokuwa nayo.

"Hii ngoma kali sana, unajua muziki wa afrobeat unazidi kuwa mkali zaidi," alisikika Rick Ross baada ya kusikiliza wimbo huo IG Live.

Navy Kenzo watakuwa wasanii wa pili kwa Mastaa nchini ambao wamewahi kufanya ngoma na Ross, ambapo wa kwanza ni Simba Diamond Platnumz ngoma ya Waka Waka (2017).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad