Ruto Azidi Kuwaumiza Wakenya 'Bei ya gesi haitashuka kama nilivyoahidi'

Rais William Ruto
William Ruto


Rais William Ruto amesema kuwa kupunguza bei ya Mitungi ya Gesi kutoka Ksh. 2800 (Tsh. 48,000) hadi Ksh.300 na Ksh.500 (Tsh. 5155 na 8592) kwa Kilogramu 6 haitawezekana ifikapo Juni 2023 kama alivyokuwa ameahidi Machi 2, 2023

Katika mahojiano ya na Waandishi wa Habari Ikulu, Jijini Nairobi, Ruto alisema idhini ya mpango huo inapaswa kutolewa katika Bajeti ya Mwaka ujao wa Fedha ambao utaanza Julai Mosi, 2023 baada ya kuwezesha Mazingira ya ufutaji wa ushuru katika Mafuta.

Amesema, "Kwanza lazima tuiidhinishe katika bajeti. Kwa sasa, hakuna njia ya kuondoa ushuru hadi bajeti mpya ipitishwe. Juni 1 haiwezekani mpaka tuipeleke Bungeni. Tutafanya pia marekebisho ya kodi inayotozwa kwenye mafuta ya taa ili kupunguza bei ya gesi."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad