Serikali Kujenga 'Flyover' Mataa ya Magomeni na Fire

 

Serikali Kujenga 'Flyover' Mataa ya Magomeni na Fire

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa leo amewasilisha Bungeni Makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo miongoni mwa mambo aliyoyasema katika hotuba yake ni mpango wa Serikali kujenga flyover za Fire na Magomeni ambapo kazi za usanifu zinaendelea.


“Katika mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) Jijini DSM na Barabara unganishi, ujenzi wa flyover ya Mbezi Mwisho umekamilika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kufanya maboresho ya makutano ya barabara kwenye maeneo ya KAMATA, Magomeni, Mwenge, Tabata/ Mandela, Fire, Selander (Ali Hassan Mwinyi/ UN Roads JCT), Buguruni na Morocco), aidha kazi za usanifu wa flyover za Fire na Magomeni zinaendelea”


“Katika mradi wa barabara za kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, mradi uliokamilika kwa mwaka 2022/23 ni ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Ardhi – Makongo – Goba (sehemu ya Ardhi – Makongo MM 5), ujezi wa barabara ya Goba – Matosa – Temboni (km 6) unaendelea kufanyika kwa awamu ambapo kilometa moja (1) imekamilika”


“Taratibu za kumpata Mkandarasi wa kipande kingine cha barabara hii zinaendelea, aidha Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Mwai Kibaki (km 9) na ujenzi wa barabara za Mjimwema – Kimbiji – Pembamnazi (km 27), Kongowe – Mjimwema – Kivukoni Ferry (km 25.1) na Kibamba – Kisopwa – Kwembe – Makondeko (km 14.66) sehemu ya Mloganzila – Kisopwa – Kwembe – Makondeko (km 10.66)”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad