Wabunge wa Tanzania wameonywa kutovua nguo zozote wanapokuwa bungeni. Spika Tulia Ackson alitoa onyo hilo baada ya Mbunge Mwita Waitara kuvua koti na tai wakati wa mjadala.
Alikuwa akionyesha kutoridhishwa na na majibu ya serikali – kuhusu fidia kwa wapiga kura wake walioko kwenye maeneo ya uchimbaji madini.
Alivua mavazi hayo huku akitoka nje ya ukumbi.
Kwa mujibu wa Spika, hakukerwa na namna ya kuondoka kwake, bali alikiuka kanuni za mavazi ya ubunge, ambayo yanahitaji uvaaji rasmi ndani ya ukumbi wa Bunge.
Alielezea kitendo chake ni kilikuwa ni “utovu wa nidhamu”.
“Tabia hii hairuhusiwi ndani ya bunge na isijirudie tena,” alisema Bi Ackson