Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC, kupitia kwa Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama, Peter Kazadi ameikabidhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tuzo ya Heshima (Gardons notre amitié) – ya kudumisha uhusiano.
Tuzo hiyo imepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini DRC, Said Mshana wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyoandaliwa kwa ajili ya Mawaziri wa SADC waliohudhuria Mkutano uliohusu
Balozi Mshana, alimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge na Uratibu katika kikao cha Mawaziri wa SADC kilichohusu udhibiti wa maafa kilichofanyika jijini Kinshasa.
Hadi kufikia Mei 25, 2023 Nchi Wanachama sita kati ya kumi na sita zilikuwa zimesaini Mkataba wa Uendeshaji wa Kituo cha Operesheni na Huduma za Kibinadamu cha SADC.