TFF yasogeza mbele Nusu Fainali ASFC



Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ limetangaza mabadiliko ya ratiba ya Mchezo wa Pili wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ kati ya Mabingwa watetezi Young Africans dhidi ya Singida Big Stars.

Mchezo huo namba 96 wa Michuano ya ASFC msimu huu 2022/23, ulipangwa kuchezwa Jumapili (Mei 07), katika Uwanja wa CCM Liti mkoani Singida na sasa utapangiwa tarehe nyingine.

Afisa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ Salum Madadi amesema sababu kubwa ya kufanyika kwa mabadiliko hayo ni kuipa muda timu ya Young Africans kujiandaa na mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

“Tulikuwa na kikao asubuhi hii lakini hatujapokea barua ya Young Africans juu ya maombi yao, lakini hii tarehe 07 mechi yao ya Azam Sports Federation na Singida Big Stars haitachezwa, Hii ni interest ya Taifa sasa tutaonana na Young Africans kujadiliana nao.”amesema Madadi


Mchezo huo wa Mkondo wa Kwanza umepangwa kufanyika Mei 10 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, na juma moja baadae Young Afrika itaelekea ugenini Afrika Kusini kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili.

Tayari Young Africans ipo mjini Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utazikutanisha timu hizo katika Uwanja wa CCM Liti mjini humo.

Mchezi huo utachezwa keshokutwa Alhamis (Mei 04), na ulitarajiwa kufuatiwa na mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania bara ‘ASFC’ ambao rasmi umeahirishwa.


Mchezo mwingine wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ utacheza Jumamosi (Mei 06) katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad