Tunajivunia Rekodi ya MONDI Youtube Ila ni Suala la Muda tu Kasi ya Burna Boy Sio Mchezo


Tunajivunia Rekodi ya MONDI Youtube Ila ni Suala la Muda tu Kasi ya Burna Boy Sio Mchezo

March 29 niliandika kuhusu staa wa Bongo Flava, Diamond Platnumz kuwa kwenye hati hati ya kuipoteza rekodi yake aliyoiweka kwa muda mrefu kwenye mtandao wa YouTube kuwa msanii mwenye views wengi zaidi kwenye mtandao huo kuliko msanii yeyote kutokea chini ya jangwa la Sahara.

Nairudisha tena baada ya kuona tunapost sana sasa hivi tukihisi, ufahari wetu ni kuwa juu ya Burna Boy, na sio uwingi wa namba.

Msanii wa pili baada ya Diamond, ni Burna Boy ambaye ndiye anakuwa tishio zaidi kutibua rekodi hii, na ni suala la muda tu. Burna Boy amekuwa na kasi ya upataji views kwenye mtandao wa YouTube hisivyo kawaida, wakati diamond anafikisha Views Bilioni 1, June 2020, Burna Boy alikuwa na Views milioni 507 (source BBC), Hii leo 2023 tunawaongelea wote wakiwa na Over 2 Billion Views.

Wakati Diamond imemchukua zaidi ya miaka miwili kupata bilioni 1 nyingine, Burna Boy ndani ya hiyo miaka miwili, amepata views bilioni 1.5, unaweza kupima kasi ya Burna Boy kwenye ongezeko la namba.

Ndani ya mwezi mmoja, March 29, 2023 hadi April 30, Diamond amekusanya views milioni 28+, wakati Burna Boy ameongeza views Milioni 55+ karibia mara mbili ya views wa Diamond. Ni suala la Hesabu tu.

Ukweli ambao wengi wetu hatutaki kuusikia, Tunawish isitokee, ila maji yanazidi unga😎.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad