Tundu Lissu "Nimeliona Gari Nililopigwa Risasi Nalo, Matundu 30 ya Risasi"


Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amekata taarifa za kuwa hatoi ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake na amesema yuko tayari kutoa taarifa na ushirikiano muda wowote atakapohitajika.

Lisu amesema hayo leo May 09,2023 akiwa Ofisi ya Polisi Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuliona gari alilotumia wakati anashambuliwa Mwezi September mwaka 2017.

“Nimeiona gari kwa mara ya kwanza na ina matundu 30 ya risasi, imenipa shida sana kwa risasi zote zile zilielekezwa kwenye mwili wa Mtu mmoja na kwasababu kumekuwa na maneno maneno kuwa Polisi wananikatalia kuchukua gari, naomba niseme wazi Polisi hawajawahi kuwa na hilo wazo na nimesema siku zote tukio hilo lichunguzwe wakiniambia nikatoe ushahidi na mimi nitafanya hivyo”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad