Twitter kuondoa akaunti ambazo hazijatumika kwa muda mrefu.



Elon Musk  siku ya jana alitoka hadharani na kutangaza kwamba atapitisha fagio na kuzisafisha/kuziondoa akaunti zote ambazo hazijatumika kwa muda mrefu. Zoezi hilo litaanza hivi karibuni.

Mkurugenzi  huyo wa Twitter alikuwa tayari ameonyesha nia ya kutaka kufuta akaunti zisizotumika Novemba mwaka jana na lisema katika mwezi uliofuata kwamba Twitter “hivi karibuni” itaanza kuachilia huru majina ya watumiaji ya akaunti bilioni 1.5, akiongeza kuwa akaunti ambazo hazitumiki zitafutwa katika mchakato huo.

“Tunasafisha akaunti ambazo hazijakuwa na shughuli yoyote kwa miaka kadhaa, kwa hivyo utaona idadi ya wafuasi ikipungua,” Bw Musk alitweet Jumatatu.

Watumiaji wengi walijibu tweet ya Bw Musk, wakiuliza ikiwa kutakuwa na njia ya kukumbuka akaunti za watumiaji waliopoteza au kusahau account zao

Bilionea huyo alidokeza kuwa akaunti zilizofutwa “zitawekwa kwenye kumbukumbu”.



Uamuzi wa hivi punde unakuja huku Twitter ikiendelea kufanya mabadiliko mapya kwenye jukwaa ili kuongeza mapato hata kama baadhi ya hatua zimewatenga watumiaji na watangazaji.

Mapema mwezi uliopita, kampuni iliondoa alama za tiki za bluu bila malipo, na kuchuma mapato katika mchakato wake wa uthibitishaji wa mtumiaji, na kuwatoza watu $8 kila mwezi kwa beji hizo

Bw Musk, hata hivyo, aliendelea kurejesha alama ya tiki kwenye baadhi ya watu mashuhuri, vyombo vya habari na akaunti nyingine za hadhi ya juu

Twitter pia imejaribu mbinu mbalimbali za kuongeza mapato, ikiwa ni pamoja na kulegeza baadhi ya sera zake zinazopiga marufuku matangazo ya kisiasa na kuongeza chaguo ghali zaidi la usajili bila matangazo kwenye jukwaa hilo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad