Vipers yaweka dau kumng'oa Mayele Yanga


Dar es Salaam. Mabingwa mara nne wa Ligi Kuu Uganda, Vipers SC wameanza na straika matata wa Yanga, Fiston Mayele ili akakipige kwenye kikosi chao msimu ujao.

Vipers SC imeanza mchakato wa kusuka kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao kwa ajili ya michuano ya CAF.

Kwa mujibu wa Pulse Sports ya nchini humo, Vipers imeshaanza na Mayele ili akakipige kwenye kikosi hicho msimu wa 2023/24.

Chanzo chao kimeeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo umeanza mazungumzo yakimuhusisha meneja wa mchezaji huyo pamoja na uongozi wa Yanga.

"Ndiyo, Vipers wameonyesha dhamira ya kumsaini Mayele kupitia wakala wake na Yanga wenyewe," kilieza chanzo hicho na kuongeza;

"Wameshaweka ofa yao ya kwanza mezani ambayo ni kati ya Dola za Marekani 50,000 (Sh117milioni) hadi Dola 100,000 (Sh230milioni) na mazungumzo yanaendelea.

"Vipers  inataka kuwa na kikosi imara wakati itakapocheza michuano ya CAF, hasa kama itashinda ubingwa wa ligi au wa Kombe la Uganda."

Ifahamike kwamba Vipers SC ni timu ya pili kucheza hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya KCCA FC iliposhiriki 2018.

Msimu huu Vipers SC ilipangwa Kundi C katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kumaliza nafasi ya mwisho wakiwa na pointi nyuma ya Horoya AC kwenye nafasi ya tatu, Simba na Raja Casablanca kwenye namba mbili na moja mtawalia, ambazo zilifuzu hatua ya robo fainali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad