Wakazi "Nilimwandikia Wimbo Roma Mkatoliki Akashindwa Kupita Nao, Wimbo wa Nipeni Maua Yangu sio Mkali"

Wakazi na Roma Mkatoliki


Rapa ROMA Mkatoliki alipotoka hadharani na kuwaomba mashabiki wampatie maua yake, alikutana na kiunzi cha Wakazi (@wakazi) ambaye hadharani aliukandia usiku mchana wimbo huo mpya kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Nini chanzo cha wawili hao kuingia kwenye msuguano? ikumbukwe sio mara ya kwanza kuwahi kutupiana maneno mitandaoni. Jana waandishi wa habari walimbana Wakazi kwenye kona na kumtaka aeleze kinaga ubaga.

Kwenye maelezo yake amefunguka juu ya ROMA (@roma_zimbabwe) kuwa mtu ambaye wanazungumza vizuri kwenye simu lakini akija mitandaoni anamsema vibaya, Wakazi alitufungulia hadi simu yake na kutuonesha ushahidi wa kuwa alimuandikia ROMA mistari lakini mkali huyo toka Tanga alishindwa kupita nayo! Wakazi ameeleza kwa upana zaidi juu ya ngoma ya ROMA na kwanini haoni kuwa ni ngoma kali, miongoni mwa sababu hizo ni kwamba wimbo huo ni mrefu sana, Wakazi amefunguka zaidi kwenye mahojiano hayo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad