Wameanza na Christiano Ronaldo, Kesho Messi.. Dunia ya Kiarabu Inayokwenda Kutawala Mchezo wa Soka Kiutani Utani



Ameandika Farhan✍️

Kuna siku nilizungumza kwenye Amplifaya ya Clouds FM, nikaita ni anguko la Ronaldo kwenye dunia isiyofahamika kwenye jengo refu jeupe! Isingekuwa rahisi kuelewana kwakuwa wengi waliishi kwenye dunia ya mpira pekee.

Dunia imegawanyika kwenye mabara mengi sana lakini kuna mabara mawili tu shindani, ni Ulaya na Asia! Lakini dunia ina taswira mbili kuu ambazo ni Wazungu na Waarabu, pande kinzani kwa kiasi chake.

Unahitaji kusoma baadhi ya vitabu vilivyoandika vyema kuhusu Waarabu na Mashariki ya kati na Uislam pamoja na dhana yake nzima! Soma kitabu cha Years of Glory, Master of the Game na Empire of Salons, vichache kati ya vingi ili upate taswira.

Bara la Asia ni kitovu cha Uislam na ndio mataifa mengi Tajiri ya Kiarabu yanapatikana hapo! Ilikuwa ni agenda kuhusu kile kinachofahamika kwenye dunia yetu kuhusu Arab Supremacy! Ni change of agenda kutoka Middle East Crisis.

Mataifa ya Mashariki ya kati yana agenda yao, kuonesha kuwa Waarabu sio Binadamu wabaya kama inavyotambulika sana na Uislam sio Uadui! Lakini rasmi wanataka kuionesha dunia kuhusu utamaduni na ustaarabu wao, kupitia michezo, twende taratibu.

Mpango kazi upo kwenye eneo la michezo ambapo michezo ikue kutoka 3.3% mpaka 8.3% ifikapo 2026! Hii World Cup Qatar sio kwa bahati mbaya, bado Formular 1 wana Bahrain, Saudi Arabia na Abu Dhabi, jumlisha GOATs Code!

Wana agenda yao kuhusu GOATs Code! Kifupi ni kusaini wachezaji wawili bora wa muda wote wakacheze Mashariki ya Kati! Tayari wana Cristiano Ronaldo ambaye mpango wake kwenda kule una visa vizito sana (Tutajadili mbele).

Kama hivyo haitoshi! Katika kuhakikisha wanaishika dunia hii, wanabadili haraka agenda kutoka Mafuta na gesi tu mpaka Utalii na michezo! Mnafahamu kuwa Lionel Messi ni Balozi wa Saudi Arabia? Unafahamu anakula pesa nyingi sana ya matangazo? Kwanini alijiamini kutoroka PSG? Tutajadili na namna ilivyokuwa.

Kumbuka ni agenda ya Mashariki ya kati, agenda ya Utamaduni wao na uislam! Tutaenda vizuri taratibu kuhusu dunia hii iliyofichika, taratibu.

ITAENDELEA….

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad